Kihongosi apendekeza adhabu kwa wakandarasi wazembe

Pendekezo lake linafuatia kutoridhishwa na kasi ya utekelezaji wa ujenzi wa Barabara za Masuliza na Kilimahewa–Tuangoma, Wilaya ya Temeke, Dar es salaam

Marion Bosire
1 Min Read

Katibu anayesimamia masuala ya itikadi, uenezi na mafunzo wa chama tawala nchini Tanzania, CCM, Kenani Kihongosi amependekza adhabu kwa wakandarasi wazembe.

Kulingana naye, wakandarasi wazembe wanapaswa kuchukuliwa hatua kwa sababu fedha zinazotumika katika ujenzi ni kodi za raia wa taifa hilo jirani la Tanzania.

Kauli ya Kihongosi inajiri baada yake kuonyesha kutoridhishwa na kasi ya utekelezaji wa ujenzi wa Barabara za Masuliza na Kilimahewa–Tuangoma, Wilaya ya Temeke, Dar es salaam zenye urefu wa kilomita 7.3 zinazojengwa na mkandarasi ambaye ni kampuni ya GroupSix International Ltd.

Katika ziara yake jana Septemba 19, 2026, Kihongosi alisema chama cha CCM na Serikali hazitaruhusu uzembe katika utekelezaji wa miradi inayotumia fedha za Wananchi.

“Kama Mkandarasi analeta mambo yasiyofaa, achukuliwe hatua na aelezwe kwamba Chama hakijaridhishwa na namna anavyofanya kazi zake katika kutengeneza hii miradi,” amesema Kihongosi.

Share This Article