Kenya na Denmark kuimarisha ushirikiano wa uwekezaji na biashara

Mudavadi alisema mataifa hayo mawili yanalenga kubuni nafasi za kazi kwa vijana na kuboresha sekta ambazo zinaimarisha moja kwa moja maisha ya raia wao.

Tom Mathinji
1 Min Read
Waziri wa Mambo ya Nje Musalia Mudavadi, ashiriki mazungumzo na balozi wa Denmark hapa nchini Stephan Schønemann.

Mkuu wa Mawaziri Musalia Mudavadi, amesema Kenya na Denmark zinaimarisha ushirikiano katika sekta za biashara na uwekezaji, ili kutoa fursa zaidi kwa raia wa nchi hizo.

Akizungumza Alhamisi aliposhiriki mazungumzo na balozi wa Denmark hapa nchini Stephan Schønemann, Mudavadi ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje, alisema mataifa hayo mawili pia yanaangazia kuboresha ushirikiano katika sekta za Afya, Utalii na Biashara, hii ikiwa ni maendelezo ya mazungumzo ya mwezi Agosti mwaka 2025.

“Baada ya miongo ya ushirikiano wa kimaendeleo katika biashara na uhusiano wa kati ya watu, lengo letu ni kuimarisha uchumi wa kidiplomasia, kuvutia uwekezaji na kupanua biashara ya Wakenya,” alisema Mudavadi.

Wakati huo huo, aliongeza kuwa mataifa hayo mawili yanalenga kubuni nafasi za kazi kwa vijana na kuboresha sekta ambazo zinaimarisha moja kwa moja maisha ya raia wao.

Share This Article