Wawili wakamatwa kwa wizi wa mita za umeme Lucky Summer, Nairobi

Martin Mwanje
1 Min Read

Polisi wamewakamata washukiwa wawili wanaotuhumiwa kuiba mita za umeme katika mtaa wa Lucky Summer jijini Nairobi.

Wakati wa msako mkali uliotekelezwa na maafisa usalama, bidhaa mbalimbali za umeme za kampuni ya Kenya Power zinazoshukiwa kuibwa pia zilipatikana.

Msako huo ulifanywa jana Jumanne na maafisa kutoka vituo vya polisi vya Lucky Summer na Ruaraka, kwa kushirikiana na maafisa wa Kenya Power.

Hii ni baada ya kupata vidokezo juu ya wizi wa mita za umeme katika eneo hilo.

Washukiwa walitarajiwa kufikishwa mahakamani leo Jumatano wakati uchunguzi kuhusiana na visa vingine ukiendelea.

Share This Article