Kiwanda cha kusafisha mafuta kufunguliwa Lamu Septemba 30

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais William Ruto, ametangaza kuwa kiwanda cha kusafisha mafuta cha  Lamu, kitazinduliwa rasmi tarehe 30 mwezi huu.

Akizungumza na Wanahabari kwenye mahojiano ya moja kwa moja kutika Ikulu ndogo ya Kisumu, kiongozi huyo wa taifa, alisema uzinduzi wa kiwanda hicho kinachojengwa na bilionea raia wa Nigeria Aliko Dangote, utahudhuriwa na Marais kadhaa wa ukanda wa Afrika Mashariki.

Wakati huo huo, Rais Ruto alisema kuna mpango wa kuunganishwa kwa bomba kutoka Lamu hadi Turkana, ili kusafisha mafuta ghafi yanayochimbwa Turkana.

 

Share This Article