Uwanja wa Talanta na ule wa Ndege wa Kisumu kupewa jina la Raila

Ruto alisema hatua hiyo inalenga kutoa heshima kwa Waziri Mkuu wa zamani aliyefariki mwaka uliopita.

Dismas Otuke
1 Min Read

Uwanja wa  michezo wa Talanta unaojengwa katika  barabara ya Ngong pamoja na uwanja wa ndege wa Kisumu,  zitabadilishwa jina na kuitwa Raila Odinga stadium na Raila Odinga International Airport mtawalia.

Haya yametangazwa na Rais William Ruto katika mahojiano ya moja kwa moja na Wanahabari wa eneo la Luo Nyanza Jumatatu jioni.

Ruto alisema hatua hiyo inalenga kutoa heshima kwa Waziri Mkuu wa zamani aliyefariki mwaka uliopita, hayati Raila Odinga.

Uwanja wa Talanta unaomudu mashabiki 60,000, utakuwa mojawapo wa viwanja viwili vikuu nchini nchini vitakavyotumika kuandaa fainali za kombe la AFCON mwaka 2027.

Share This Article