Wakulima kote nchini wametakiwa kutumia mpango wa mbolea ya ruzuku uliotangazwa na Rais William Ruto kununua mbolea hiyo ya bei nafuu ili kuimarisha mazao yao msimu ujao wa upanzi.
Kwenye mpango huo, bei ya gunia la kilo 50 la mbolea imepunguzwa kutoka shilingi 2,500 hadi 2,000.
Katibu katika Idara ya Magereza Dkt. Salome Beacco amewataka wakulima kutumia mpango huo kununua mbolea hiyo kwa lengo la kuboresha uzalishaji wa mazao.
Akizungumza katika kaunti ya Taita Taveta Agosti 24, Rais Ruto aliashiria kuwa bei hiyo mpya itaanza kutekelezwa ndani ya kipindi cha majuma, ikiwa na maana bei hizo tayari zimetekelezwa.
Aliwataka wakulima kutumia fursa hiyo kuboresha kilimo chao msimu ujao wa upanzi.
Aidha, Rais alitangaza kuwa serikali itapunguza bei ya mbegu ya mahindi kwa asilimi 50.
Mbolea ya ruzuku imekuwa ikiuzwa kwa shilingi 2,500 tangu mwanzo wa utawala wa Rais Ruto kutoka bei ya awali ya shilingi 5,000.