Safari ya Gor Mahia katika Ligi ya Mabingwa Afrika ilifikia tamati ghafla bin vuu baada ya kuambulia kichapo cha mabao 5-1, na Pyramids ya Misri katika marudio ya mchujo wa kwanza katika uwanja wa June 30 jijini Cairo.
Walid El Karti,Nasser Maher,Youssef Obama, walipachika bao moja kila mmoja katika kipindi cha kwanza naye David Okoth, akakomboa goli moja dakika ya 45.
Mostafa Ziko anaye alitikisa nyavu mara mbili dakika ya 90 na 94 kuawapa ushindi maridhawa.
Gor walikuwa wamepoteza mabao magoli 2 kwa bila katika uwanja wa Nyayo katika duru ya kwanza.
Gor
Pyramids walifuzu kwa mchujo wa pili kwa ushindi wa jumla wa mabao 7-1 ,na sasa watakabiliana na El Merreikh Bentiu ya Sudan Kusini.
K’ogalo nao watarejea nyumbani kuanza kujipanga kutetea taji ya Ligi kuu katika msimu ulioratibiwa kung’oa nanga Jumamosi hii.