Kenya yaambulia patupu Budapest ,Wanyonyi amaliza wa tatu

Wanyonyi alivuka mstari wa mwisho kwa muda wa dakika 1 sekunde 42.44.

Dismas Otuke
1 Min Read
BUDAPEST, HUNGARY - SEPTEMBER 13: Djamel Sedjati of Team Algeria reacts as he crosses the finish line to win the Men's 800 Metres Final during Day 3 of the World Athletics Ultimate Championship at National Athletics Centre on September 13, 2026 in Budapest, Hungary. (Photo by Mattia Ozbot/World Athletics via Getty Images)

Matumaini ya Kenya kutwaa angaa  ubingwa mmoja katika makala ya kwanza ya mashindano ya Dunia ya Ultimate mjini Budapest,Hungary yametumbukia nyongo baada ya bingwa wa dunia na Olimpiki Emmanuel Wanyonyi kumaliza wa tatu katika fainali ya mita 800.

Wanyonyi alivuka mstari wa mwisho kwa muda wa dakika 1 sekunde 42.44.

Djamel Sedjaati wa Algeria alitoka nyuma na kutwaa ubingwa kwa dakika 1 sekunde 41.91,mbele ya Marco Arop wa Canada aliyemaliza wa pili.

Awali, Julius Yego alimaliza wa sita katika urushaji sagai alirusha umbali wa mita 80.23, huku Rumesh Pathrage wa Srilanka akishinda kwa kurusha mita 91.09.

Timothy Cheruiyot na Phanuel Kosgei wamemaliza katika nafasi za nane na kumi katika mita 1500,mbio zilizoshindwa  na Josh Kerr.

 

Share This Article