Tusker FC wamewashinda wageni Al Ahli Wad Madani FC, kutoka Sudan bao 1-0, katika marudio ya mchujo wa kwanza kuwania kombe la shirikisho la soka Afrika.
Mechi hiyo ya Jumamosi alasiri katika uwanja wa kitaifa wa Nyayo ilishuhudia timu zote zikijihami huku kipindi cha kwanza kikimalizikia sare tasa.
Hata hivyo Erastus Erambo, alipata pasi murua kunako dakika ya 62 na kupachika bao pekee na la ushindi.
Tusker wamefuzu kwa mchujo wa pili kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-2 ,baada ya duru ya kwanza kuishia sare ya 2-2 wiki jana.
Wanabururi watachuana na Singida Black Stars ya Tanzania, katika mchujo wa pili huku mshindi wa jumla akijikatia tiketi kwa hatua ya makundi.