Marekani ilitawala siku ya kwanza ya mashindano ya Riadha ya Ultimate, yanayoandaliwa kwa mara ya kwanza mjini Budapest,Hungary,Ijumaa usiku.
Wanariadha wa Marekani walishinda fainali tatu kati ya nane zilizoandaliwa.
Marekani ilitwaa ubingwa wa mita 100 kwa wanariadha wanne kupokezana kijiti,jinsia mchanyato,mita 11o na mita 100 kuruka vizuizi kwa wanaume na wanawake.
Gwiji wa urukaji kwa upote kwa wanaume Armaund Duplantis wa Uswidi alinyakua ubingwa ,wakati Yaroslav Makhuchikh wa Ukrain akishinda urukaji kimo kwa wanawake ,naye Merlin Hummel kutoka Ujerumani akishinda urushaji nyundo.
Washindi wengine wa Ijumaa usiku walikuwa Larisa Iapichino wa Italia aliyeshinda urukaji mapana huku Jakob Ingebrigsten wa Norway akishinda mita 5,000 wanaume.
Makala hayo ya kwanza yanawashirikisha Mabingwa wa Olimpiki mwaka 2024,Mabingwa wa dunia mwaka 2025 na Mabingwa wa Diamond League msimu huu.