Kenya inatarajiwa kupokea shilingi bilioni 51.8 fedha za dharura kutoka kwa benki ya Dunia, kukabiliana na mikasa na majanga kama vile El Niño, kuzuka kwa ugonjwa wa Ebola katika ukanda huu na gharama za juu za umeme.
Taifa hili litapokea fedha hizo ndani ya muda wa majuma sita, huku msemaji wa benki ya Dunia akidokeza kuwa zitaisaidia serikali kukabiliana na majanga.
Kenya ilikuwa imetuma maombi ya fedha hizo kufuatia vita vya Iran mwezi Februari mwaka huu, hali iliyopandisha bei ya mafuta ghafi.
Miradi itakayonufaika na pesa hizo ni pamoja na kukabiliana na mvua ya El Niño inayotarajiwa kuanzia mwezi Oktoba na athari zake kwa kilimo pamoja na raslimali za maji.
Aidha, fedha hizo zitasaidia serikali kukabiliana na makali ya kupanda kwa bei ya mafuta duniani na kuzuka kwa ugonjwa wa Ebola .