Taasisi ya kuwateua wanafunzi wa kidato cha nne wanaopaswa kujiunga na vyuo vikuu na vile vya kiufundi nchini Kenya (KUCCPS), imesimama kidete na kutoa orodha ya wanafunzi walioteuliwa kujiunga na vyuo mbalimbali kwa vyuo ambayo vilivyo na malimbikizi ya madeni.
KUCCPS imesema itatoa orodha hiyo kwa vyuo pekee vilivyowalisha pesa zinazohitajika au kutoa mpango wa kulipa madeni hayo.
Kwa kawaida vyuo hutoza kila wanafunzi ada za shilingi 1,500 za usajili zinazolipwa wakati mwanafunzi huingia chuoni ambazo zapaswa kuwasilishwa kwa KUCCPS.
Hata hivyo KUCCPS inadai vyuo jumla ya deni la shilingi nusu bilioni kutoka kwa vyuo vikuu na vile vya kiufundi.