Kenya, Italia zatia saini mkataba wa ujenzi wa hospitali 15 mpya

Rais William Ruto alisema ushirikiano huo utafanikisha ujenzi wa hospitali 13 za kiwango cha level 5 na hospitali mbili za rufaa na mafunzo katika kaunti 15.

Tom Mathinji
1 Min Read
Kenya na Italia zatia saini mkataba wa ujenzi wa hospitali 15 mpya nchini Kenya.

Serikali za Kenya na Italia kwa ushirikiano na kampuni ya GKSD, zimetia saini makubaliano ya ujenzi wa hospitali 15 mpya kote nchini Kenya.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Rais William Ruto alisema ushirikiano huo utafanikisha ujenzi wa hospitali 13 za kiwango cha level 5 na hospitali mbili za Rufaa na Mafunzo katika kaunti 15.

“Chini ya ushirikiano huu, tutajenga hospitali 13 za level 5 na hospitali mbili za Rufaa na Mafunzo katika kaunti 15,” alisema Rais Ruto.

Kiongozi wa taifa alisema hospitali hizo mpya zitapanua uwezo wa hospitali wa Kenya, zitaleta huduma za matibabu za kitaalam karibu na wananchi, na kuchochea upatikanaji wa huduma za afya kwa wote (UHC).

Ruto alisema miradi hiyo inayotekelezwa chini ya mpango wa Matei barani Afrika, itabadilisha maisha ya Wakenya.

Share This Article