Adama Barrow: Serikali inashughulikia ukosefu wa unguvu za umeme

Waandamani ambao waliteketeza magurudumu na kufunga barabara katika Jiji Kuu Banjul Jumatatu na Jumanne, wanashinikiza kujiuzulu kwa Rais Barrow.

Tom Mathinji
1 Min Read
Adama Barrow - Rais wa Gambia.

Rais wa Gambia Adama Barrow, amesema taifa hilo litaimarisha usambazaji wa nguvu za umeme kufikia mwezi ujao, huku maanadmano yakishuhudiwa kote nchini humo kutokana na ukosefu wa umeme kwa muda mrefu.

Waandamani ambao waliteketeza magurudumu na kufunga barabara katika Jiji Kuu Banjul Jumatatu na Jumanne, wanashinikiza kujiuzulu kwa Rais Barrow.

Maafisa wa Polisi walitumia gesi ya kutoa machozi kutawanya waandamanji ambao pia walikuwa wamekusanyika karibu na makao ya Rais Barrow na katika Makao Makuu ya Shirika la Maji na Umeme (NAWEC), ambalo husambaza umeme kote nchini humo.

Kwenye hotuba yake kwa taifa, Rais Barrow alitangaza kuwa serikali itajenga kiwanda cha umeme kinachotumia miale ya jua cha megawati 24, kufikia mwisho wa mwezi wa Oktoba.

Ukosefu wa nguvu za umeme katika taifa hilo la Afrika Magharibi umejiri wakati wa msimu wa joto na umedumu hadi saa 48 katika baadhi ya maeneo.

Share This Article