Polisi wasambaratisha biashara ya pombe haramu Kahawa West

Maafisa hao walinasa na kuharibu lita  3,200 za pombe haramu aina ya kangara, lita 45 za changaa, lita 10 za muratina na vifaa kadhaa vya kugema.

Tom Mathinji
1 Min Read
Polisi wasambaratisha biashara ya pombe haramu Kahawa West.

Maafisa wa Polisi wamesambaratisha mtandao wa biashara ya uuzaji na usambazaji wa pombe haramu katika kaunti ndogo ya Kasarani, jijini Nairobi.

Kwenye operesheni hiyo ya kijasusi iliyotekelezwa Septemba 7, 2026, maafisa hao walinasa na kuharibu lita  3,200 za pombe haramu aina ya kangara, lita 45 za changaa, lita 10 za muratina na vifaa kadhaa vinavyotumika katika shughuli za ugemaji.

Kulingana na Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), mshukiwa anayedaiwa kutekeleza biashara hiyo haramu alikamatwa na anazuiliwa kwenye korokoro za polisi akisubiri kufikishwa mahakamani.

Huduma ya Taifa ya Polisi, ilielezea kujitolea kwake kuendeleza operesheni kote nchini, kukabiliana na ulanguzi wa mihadarati na pombe haramu.

“Tunawahmiza wananchi kuendelea kutoa habari kwa maafisa wa usalama kuhusu shughuli wanazotilia shaka,” ilisema DCI.

Share This Article