Cameroon imemaliza tena katika nafasi ya tatu na kujishindia nishani ya shaba katika mashindano ya Voliboli kwa wanawake barani Afrika baada ya kuwashinda Rwanda seti tatu kwa bila.
Cameroon walipata ushindi katika mechi hiyo iliyoandaliwa Ijumaa katika ukumbi wa Kasarani kwa seti za 25-17, 25-16 na 25-19, huku mechi hiyo ikidumu kwa saa 1 na dakika 11 pekee.
Kufuatia matokeo hayo Cameroon,Kenya na Misri zimefuzu kwa mashindano ya Dunia mwaka ujao.
Mabingwa wa mashindano hayo watafuzu kwa michezo ya Olimpiki ya mwaka 2028 nchini Marekani.