Rekodi ya Wanyonyi yarasimishwa

Wanyonyi  ambaye ni Bingwa wa Olimpiki na aliye na umri wa miaka 20, alivunja rekodi ya miaka 27 ya dakika 2 sekunde 11.96, iliyoandikishwa na Mkenya mwenza Noah Ngeny, mjini Rietti Italia,Septemba 5 mwaka 1996.

Dismas Otuke
1 Min Read

Shirikisho la Riadha Ulimwenguni limerasimisha rekodi ya Dunia ya mbio za Mita 1,000 ya dakika 2 sekunde 11.83 ya Mkenya Emmanuel Wanyonyi.

Wanyonyi  ambaye ni Bingwa wa Olimpiki na aliye na umri wa miaka 20, alivunja rekodi ya miaka 27 ya dakika 2 sekunde 11.96, iliyoandikishwa na Mkenya mwenza Noah Ngeny, mjini Rietti Italia,Septemba 5 mwaka 1996.

Aidha, Shirikisho la Riadha Ulimwenguni limeidhinisha rekodi ya nusu marathoni ya dakika 57 na sekunde 20, yake Mganda Jacob Kiplimo, katika mbio za Lisbon mwezi Machi mwaka huu.

Hata hivyo rekodi ya Kiplimo ilivunjwa maajuzi na Mwethiopia Yomif Kejelcha, ingawa haijaidhinishwa.

Share This Article