Wafanyabiashara wa kigeni na wachuuzi wasio na leseni kufurushwa

Maafisa waserikali wametakiwa kutathmini na kurekebisha misingi ya kutoa leseni kwa wafanyabiashara wa kigeni humu nchini.

Dismas Otuke
1 Min Read

Serikali imetangaza kuanza msako wa kuwafurusha wafanyabiashara wa kigeni na wachuuzi wasio na leseni kuanzia Septemba 7.

Akitangaza hatua hiyo  Jumatano jioni katika Ikulu ya Nairobi alipokutana na wawekezaji, Rais William Ruto alisema ni jukumu la serikali kuwalinda wafanyabiashara dhidi ya ushindani usio halali.

Aliongeza kuwa tayari mswada uko bungeni ambao ukipitishwa, utazuaia raia wa kigeni kufanya  biashara fulani zinazostahili kufanywa na Wakenya pekee.

Aidha, aliwataka maafisa wa serikali kutathmini na kurekebisha misingi ya kutoa leseni kwa wafanyabiashara wa kigeni humu nchini.

 

Share This Article