Serikali ya Tanzania imetangaza bei mpya za mafuta ya Petroli na Dizeli zitakazotumika mwezi huu wa Septemba.
Kulingana na mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji (EWURA) bei mpya ya Petroli imeshuka kwa shilingi 4.98, sawa na shilingi 102 za Tanzania huku ile ya Dizeli ikiuzwa kwa 4.93, sawia na shilingi 101 kwa kila lita moja.
EWURA imetangaza kuwa lita moja ya Petroli jijini Dar es Salaam itakuwa shilingi 3,796 za Tanzania sawa na shilingi 185.39, huku Dizezli ikiuzwa kwa shilingi 3,877 za Tanzania sawia na shilingi 189.34 za Kenya.
Serikali hata hivyo,imewaonya wenye mafuta kutoongeza bei wala kuuza bidhaa hiyo kwa za chini kuliko zilizowekwa na Ewura.
Bei hizo zinatarajwia kuzuia kupanda kwa gharama za usafiri kwa kutumia magari ya umma.