Rais William Ruto amewaaga Mabalozi wa Ufaransa na Ethiopia, waliokamilisha muda wao wa kuhudumu humu nchini.
Akimuaga Balozi wa Ufaransa humu nchini Arnaud Suquet,Ruto alielezea uhusiano wa karibu wa Kidiplomasia kati ya Kenya na Ufaransa.
Alitaja mafanikio makubwa ya maandalizi ya kongamano la Africa Forward Summit, kilichohudhuriwa na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron mwezi Mei ambapo Balozi huyo aliwajibika pakubwa .
Aidha, ilikuwa mara ya kwanza kwa kongamano hilo kuandaliwa nje ya Ufaransa na barani Afrika, ambapo Kenya ilitia saini ushirikiano wa kibiashara ikiwemo ukarabati wa reli ya Nairobi kwa kima cha shilingi bilioni 12.5.
Balozi huyo anaondoka nchini baada ya kukamilisha muhula wake wa kuhudumu wa miaka minne.
Wakati uo huo Ruto, amemwaga Balozi wa Ethiopia humu nchini Bacha Debele Buta ambaye pia amekamilisha kipindi chake cha kuhudumu.