Muthoni: Serikali imeimarisha usalama wa afya mipakani

Tom Mathinji
1 Min Read
Katibu wa afya ya Umma Mary Muthoni.

Katibu katika Idara ya Afya ya Umma Mary Muthoni, amesema serikali inahakikisha taratibu zote za kuwachunguza wasafiri mipakani zinafuatiliwa kikamilifu.

Akizungumza Jumamosi alipozuru kituo cha mpakani cha Busia kukadiria mifumo iliyopo ya kudhibiti ugonjwa wa Ebola, Muthoni alisema Wizara ya Afya iko makini kuimarisha uchunguzi, kufanikisha uzingatiaji wa itifaki za afya ya umma na ushirikiano wa asasi mbalimbali ili kuzia ugonjwa huo kuingia hapa nchini.

“Serikali imejitolea kuimarisha usalama wa afya mipakani, huku ikiwezesha usafiri salama wa watu na bidhaa mipakani,” alisema Muthoni.

Aidha, katibu huyo aliwapongeza wahudumu wa afya, maafisa wa mipakani na asasi za washirika kwa juhudi zao za kuchunguza na uwezo wa kukabiliana chamko la ugonjwa huo.

Alisema wameimarisha uwezo wa baadhi ya maabara kuchunguza ugonjwa huo, ambazo zinajumuisha maabara ya KEMRI Nairobi, KEMRI Kisumu na vifaa vya uchunguzi vya kuhamahama.

Share This Article