Rais Xi asema China na Misri zinatoa mfano wa urafiki na mshikamano kati ya nchi zinazoendelea

Rais Xi ametoa salamu za dhati na matumaini mema kwa serikali na watu wa Misri kwa niaba ya serikali ya China na watu wake.

KBC Digital News
1 Min Read

Rais Xi Jinping wa China amesema China na Misri zimetoa mfano wa urafiki, mshikamano na uratibu kati ya nchi zinazoendelea, zikiwa na kiwango kikubwa cha kuaminiana kisiasa, ushirikiano wa kunufaishana, na uratibu wa karibu na wenye ufanisi katika mambo ya pande nyingi.

Rais Xi amesema hayo kwenye hotuba ya maandishi aliyoitoa wakati alipowasili huko Cairo kwa ziara ya kiserikali nchini Misri kutokana na mwaliko wa Rais Abdel Fattah El-Sisi wa Misri.

Rais Xi ametoa salamu za dhati na matumaini mema kwa serikali na watu wa Misri kwa niaba ya serikali ya China na watu wake.

Rais Xi amesema China na Misri zote ni staarabu za kale, zikiwa na urafiki wa jadi ambao umedumu kwa maelfu ya miaka na kupitia mtihani wa wakati.

Amesema katika miaka 70 iliyopita tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia, nchi hizo mbili siku zote ziko pamoja na zimetafuta ushirikiano wa kunufaishana bila kujali mabadiliko ya hali ya kimataifa na kikanda.

Taarifa ya CGTN

 

Share This Article