Kenya kukabiliana na Cameroon nusu fainali ya Voliboli ya wanawake Afrika

Nusu fainali ya kwanza itakuwa kati ya Misri na Rwanda kuanzia saa kumi baada ya Rwanda kuwatema Ghana seti 3-1 huku Misri ikiwabandua Tunisia seti 3-0.

Dismas Otuke
1 Min Read

Wenyeji Kenya watachuana na Cameroon katika nusu fainali ya Kombe la Afrika Alhamisi hii huku wakilenga kutetea kombe hilo.

Malkia Strikers walifuzu kwa nusu fainali kufuatia ushindi wa seti 3-1 dhidi ya Algeria Jumanne usiku katika ukumbi wa Kasarani.

Kenya ilipoteza seti ya kwanza  21-25, kabla ya kutwaa seti zilizofuatia 25-7,25-15 na 25-18, na kujikatia tiketi kwa nusu fainali.

Cameroon walifuzu kwa nusu fainali kufuatia ushindi wa seti 3-0 dhidi ya Uganda.

Nusu fainali ya kwanza itakuwa kati ya Misri na Rwanda kuanzia saa kumi baada ya Rwanda kuwatema Ghana seti 3-1 huku Misri ikiwabandua Tunisia seti 3-0.

Fainali ya mashindano hayo ni Jumamosi hii huku washindi wakifuzu kwa mashindano ya Dunia mwaka ujao na pia Michezo ya Olimpiki ya mwaka 2028.

 

Share This Article