Kipute cha Voliboli ya vidosho Afrika kuingia robo fainali leo

Saa kumi alasiri, itakuwa zamu ya derby ya Afrika Kaskazini, Tunisia wakipimana ubabe na Misri kisha wenyeji Kenya wafunge kazi saa moja dhidi ya Algeria.

Dismas Otuke
1 Min Read

Kindumbwendumbwe cha Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Voliboli ya wanawake kitaingia hatua ya robo fainali leo Jumanne katika ukumbi wa Kasarani jijini Nairobi.

Uganda watafungua raundi hiyo ya nane bora kwa kukwangurana na Cameroon saa nne asubuhi, kabla ya kuwapisha Rwanda watakaovaana na Ghana saa saba mchana.

Saa kumi alasiri, itakuwa zamu ya derby ya Afrika Kaskazini, Tunisia wakipimana ubabe na Misri kisha wenyeji Kenya wafunge kazi saa moja dhidi ya Algeria.

Mechi za nusu fainali zitasakatwa baina ya Septemba 3 na 4 huku fainali ikichezwa Jumamosi hii.

Share This Article