Wafanyakazi wa viwanja vya ndege nchini wamesitisha mgomo mapema Jumanne Seotemba mosi, baada ya kutia saini makubaliano ya kurejea kazini Jumatatiu usiku.
Chama cha wafanyakazi hao KAWU kimisitisha mgomo baada ya kuafikiana na Mamlaka ya usimamizi wa viwanja wa ndege nchini KAA,shirika la wahandisi wa ndege KAA na kampuni ya ndege ya Jambojet.
KAWU imesema kuwa itaanza mazungumzo mara moja kuhusu nyongeza ya mshahara kwa wafanyakazi.
Mgomo huo ulisitisha shughuli zote katika viwanja vya ndege nchini Kenya,huku wasafiri wakikwama katika uwanja mkubwa wa kimataifa wa Jomo Kenyatta, wakati pia ndege zikilazimika kufutilia mbali safari zote.
Wafanyakazi wote wametakiwa kurejea kazini huku usafiri ndege ndani na nje ya Kenya ukitarajiwa kurejelewa.
KAWU wamekubaliana kuhusu matakwa kadhaa na serikali ikiwemo kutoadhibiwa kwa wote waliohusika kwenye mgomo huo.
Mwafaka huo umepatikana kufuatia mazungumzo ya muda mrefu Jumatato jioni kati ya maafisa wa KAWU,KCAA,KAA ,na Jambo jet ,ukiongozwa na Waziri wa Uchukuzi Davies Chirchir na Katibu Mkuu wa chama cha wafanyakazi nchini (COTU) Francis Atwoli.