Wakenya walioathiriwa ajali ya ndege Ethiopia, kupata shilingi milioni 353

Maafikiano hayo yanamaliza mzozo wa mahakamani uliodumu kwa miaka saba na Boeing watalipa familia za Wakenya walioathiriwa jumla ya shilingi bilioni 11.3 kama ridhaa.

Dismas Otuke
1 Min Read

Kila familia za Wakenya 32 walioangamia katika mkasa wa ajali ya ndege ya Ethiopia mwaka 2019, itapokea ridhaa ya shilingi milioni 353.

Hii inafuatia makubaliano nje ya mahakama mwaka jana baina ya Kampuni ya Boeing na idara ya haki nchini Marekani, ambayo iliondoa hukumu dhidi ya kampuni hiyo ya kutengeza ndege.

Maafikiano hayo yanamaliza mzozo wa mahakamani uliodumu kwa miaka saba na Boeing watalipa familia za Wakenya walioathiriwa jumla ya shilingi bilioni 11.3 kama ridhaa.

Ndege hiyo aina ya Boeing 373 MAX iliyokuwa ikitoka katika uwanja wa ndege wa Bole nchini Ethiopia, ikielekea uwanja wa ndege wa Jomo kenyatta,Nairobi,ilianguka katika eneo la Bishoftu nchini Ethiopia ,dakika sita sita tu baada ya kupaa na kuwaua abiria wote 149 na wahudumu 8.

Share This Article