Bintiye Rais Museveni asimikwa kuwa Kasisi wa kwanza mwanamke Uganda

Rais Museveni na Mkewe Janet Museveni walihudhuria hafla hiyo ya kufana na ya kihistoria.

Dismas Otuke
1 Min Read

Bintiye Rais wa Uganda Yoweri Museveni, Patience Kokundeka Robwogo Museveni, amesimikwa kuwa kasisi wa kwanza mwanamke nchini Uganda.

Hafla ya kusimikwa kwa Kasisi Rwobogo, ilifanyika Jumapili iliyopita katika kanisa la Covenant Hill Maya katika wilaya ya Wakiso,ikiambatana na maadhimisho ya miaka 20 tangu aanzishe kanisa hilo.

Aidha, Rwabogo anakuwa mwanamke wa kwanza kusimikwa kuwa Kasisi wa kanisa hilo na pia nchini Uganda.

Rais Museveni na Mkewe Janet Museveni walihudhuria hafla hiyo ya kufana na ya kihistoria.

Share This Article