Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka, IEBC imechapjsha notisi ya Uchaguzi Mkuu 2027, ikiwa imesalia takriban mwaka mmoja kabla ya uchaguzi huo kuandaliwa.
Kwa mujibu wa ratiba hiyo, Uchaguzi Mkuu ujao umeratibiwa kuandaliwa Agosti 10, 2027.
Afisa yeyote wa umma anayekusudia kujitosa siasani anahitajika kujiuzulu kufikia Februari 10 mwakani.
Kwa upande mwingine, kampeni za uchaguzi huo zitaanza rasmi Mei 29 na kumalizika Agosti 7, siku mbili kabla ya kuandaliwa kwa uchaguzi kwa mujibu wa sheria.
Wakati wanasiasa wakiwa tayari wameanza kuwinda kura kuelekea uchaguzi huo, IEBC inasema kufanya kampeni nje ya kipindi hicho ni ukiukaji wa sheria.
Usajili wa wagombe wote utafanyika Mei 2 hadi Juni 11, 2027 ukijumuisha wagombea wa Urais, Ubunge, Useneta, Magavana, Wawakilishi wa Wanawake na Wawakilishi Wadi.