Serikali yatoa onyo kali kwa watengenezaji saruji Tanzania

Serikali ilitoa makataa hayo siku ya Jumatano baada ya kukutana na wenye viwanda vinavyotengeza saruji.

Dismas Otuke
0 Min Read

Watengenezaji wa saruji nchini Tanzania wamepewa makataa ya siku nane kumaliza uhaba wa bidhaa hiyo muhimu na kupunguza bei.

Serikali ilitoa makataa hayo siku ya Jumatano baada ya kukutana na wenye viwanda vinavyotengeza saruji.

Inaaminika kuwa uhaba wa sarauji katika maeneo mengi umesababisha bei kupanda hadi shilingi 26,000 kwa kila mfuko wa kilo 50 sawa na shilingi 1,271 za Kenya.

Share This Article