Kipyegon kukosa kushiriki mashindano yote mwaka huu

Kupitia kwenye ukurasa wake wa X Kipyegon alisema, “Tangu mwezi Mei, nimekuwa nikikabiliana na jeraha la paja lakini kwa bahati mbaya linahitaji muda mrefu zaidi kabla ya kupona.”

Dismas Otuke
1 Min Read

Bingwa mara tatu wa Olimpiki katika mbio za mita 1500 Faith Kipyegon, hatashiriki tena kwenye mashindano yoyote mwaka huu kutokana na jeraha la mguu.

Kipyegon ambaye pia ni bingwa mara nne wa Dunia katika mbio za mizunguko mitatu unusu, ametangaza kuwa jeraha alilokuwa akiuguza tangu mwezi Mei limechukua muda mrefu kupona, hivyo basi hana budi kujiondoa katika mashindano yote yaliyosalia mwaka huu.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa X, Kipyegon alisema “Tangu mwezi Mei, nimekuwa nikikabiliana na jeraha la paja lakini kwa bahati mbaya, linahitaji muda mrefu zaidi kabla ya kupona.”

Hatua hii ina maana kuwa mwanariadha huyo aliye na umri wa miaka 32, atakosa mashindano yaliyosalia ya Diamond League na pia makala ya kwanza ya mashindano ya Ultimate Championships, yatakayoandaliwa mjini Budapest nchini Hungary mwezi ujao.

Share This Article