Jeshi la Uganda kuandaa mashindano baina ya vikosi

Fainali ya mashindano hayo itahudhuriwa na mshauri wa Rais wa masuala ya kijeshi  Jenerali Kainerugaba Muhoozi Agosti 25.

Dismas Otuke
1 Min Read

Jeshi la Uganda, UPDF litaandaa mashindano ya mwigo wa kivita katika  uwanja wa Uhuru wa Kololo viungani mwa mji wa  Kampala.

Zoezi hilo litakaloshirikisha wanajeshi zaidi ya 1400 kutoka timu 40 za vikosi vyote vya jeshi litaandaliwa kati ya Agosti 22 na 25.

Timu 5 bora pia zitashiriki mashindano ya mtindo  huria ambao unajumuisha ubunifu, uweledi na tamaduni za Kiganda.

Fainali ya mashindano hayo itahudhuriwa na mshauri wa Rais wa masuala ya kijeshi  Jenerali Kainerugaba Muhoozi Agosti 25.

TAGGED:
Share This Article