Tanzania na DRC zaafikiana kutanua biashara kupitia bandari ya Dar

Kwa sasa, nchi hizo mbili hufanya biashara ya kima cha shilingi bilioni 794 za Tanzania sawa na bilioni 38.4 za Kenya kupitia bandari ya Dar es Salaam.

Dismas Otuke
1 Min Read

Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC zimeafikiana kupanua biashara  kupitia kwa bandari ya Dar es Salaam kutoka kiwango cha sasa.

Mataifa hayo mawili yaliafikiana baada ya kutia saini makubaliano kufuatia kikao cha pamoja kati ya maafisa wa serikali za DRC na Tanzania.

Kwa sasa, nchi hizo mbili hufanya biashara ya kima cha shilingi bilioni 794 za Tanzania sawa na bilioni 38.4 za Kenya kupitia bandari ya Dar es Salaam.

Haya yanajiri huku Rais wa DRC Felix Tshisekedi akizuru Tanzania kwa ziara rasmi ya kiserikali ya siku mbili, ambapo alikutana na mwenyeji wake Dkt. Samia Suluhu Hassan siku ya Jumanne.

Mataifa hayo aidha yanalenga kuunganisha barabara, reli na bandari ili kurahisisha usafirishaji wa mizigo.

Share This Article