Hatima ya kesi inayomkabili kiongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) Tundu Lissu itabainika Ijumaa hii Agosti 21.
Mahakama ya Dar es Salaam inatarajiwa kutoa uamuzi siku ya Ijumaa endapo Lissu ana kesi ya kujibu au la katika kesi ya uhaini inayomkabili.
Jumla ya mashahidi 17 kati ya 30 walikuwa wametoa ushahidi kufikia Jumatatu wiki hii kulingana na kiongozi wa mashtaka.
Lissu anakabiliwa na kesi ya uhaini na kujaribu kusimamisha uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.