Kesi inayomkabili mwanasiasa mkongwe nchini Uganda, Dkt. Kizza Besigye na washirika wake Hajj Obeid Lutale na Denis Oola, imerejelewa leo Jumanne jijini Kampala ingawa Besigye hakuwepo mahakamani.
Watatu hao wanakabiliwa na makosa ya uhaini.
Kukosa kufika mahakamani kwa Besigye kunajiri baada kuanguka na kuzirai Julai 29 ndani ya mahakama wakati wa kusikizwa kwa kesi yake.
Baadaye, alipekekwa katika hospitali ya rufaa ya Mulago alikolazwa kwa siku 10 akiwa katika kitengo cha wagonjwa wanaojitegemea (HDU) na baadaye kuhamishiwa hospitali ya Luzira Prisons Agosti 7.
Ingawa taarifa kamili haijatolewa, yamkini afya ya mwanasiasa huyo haiko shwari, hali iliyomfanya kutofikishwa mahakamani.