Wizara ya Fedha yaangazia maendeleo ya mageuzi

Martin Mwanje
1 Min Read
Dkt. Chris Kiptoo - Katibu katika Wizara ya Fedha

Katibu katika Wizara ya Fedha Dkt. Chris Kiptoo leo Jumatatu amewaongoza Wakurugenzi Wakuu na Wakuu wa Idara kupigia msasa hatua zilizopigwa katika kutekeleza mageuzi muhimu na mipango ya kimkakati katika wizara hiyo. 

Wakati wa mkutano huo wa kimkakati wa siku moja, kila kurugenzi inaelezea hatua iliyopiga chini ya madaraka yake, changamoto ilizokumbana nazo, vipaumbele na nyanja zinazohitaji ushirikiano thabiti.

Mazungumzo yakiangazia namna ya kuzikabili changamoto ibuka, kuimarisha uwajibikaji na kuboresha shabaha ya wizara hiyo katika kutoa huduma bora.

“Lengo la mkutano ni kuimarisha utekelezaji, kuharakisha matokeo na kutoa athari kubwa,” alisema Dkt. Kiptoo

 

Share This Article