Cameroon walitawazwa mabingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika (WAFCON) kwa mara ya kwanza baada ya kuwazabua limbukeni Malawi mabao 3-0 kwenye fainali iliyosakatwa Jumapili usiku uwanjani Prince Moulay jijini Rabat, Morocco.
Marie Ngah aliwaweka kifua mbele Indomitable Lionesses kunako dakika ya 20 kufuatia utepetevu wa mabeki wa Malawi.
Naomi Ndjoah Eto alitanua uongozi wa Cameroon kwa goli la pili dakika ya 30, kabla ya Ngah kuongeza la pili na kuongoza 3-0 kufikia mapumzikoni.
Aidha, Cameroon, Malawi, Morocco na Algeria zilifuzu kwa fainali za Kombe la Dunia mwaka ujao nchini Brazil kwa kucheza hadi nusu fainali.
Algeria ilimaliza ya tatu kufuatia ushindi wa mabao 3-2 kupitia penalti dhidi Morocco kufuatia sare ya bao moja.
Nigeria wameshinda kombe hilo mara 10, Equitorial Guinea mara mbili huku Afrika Kusini na Cameroon wakinyakua kombe moja kila moja.
Jumla ya mataifa 16 yalishiriki makala ya mwaka huu huku Kenya ikicheza kwa mara ya pili.