Mchezaji soka maarufu Stéphane Aziz Ki amerejea kwenye timu yake ya awali nchini Tanzania ya Young Africans SC almaarufu Yanga SC.
Klabu hicho cha soka kilitangaza kurejea kwake kupitia akaunti zake za mitandao ya kijamii ambapo picha yale ilichapishwa ikiwa na maandishi, “Amerejea. Karibu nyumbani Aziz Ki”.
Aziz aliwahi kuchezea Yanga SC awali kati ya mwaka 2022 na 2025 kabla ya kuhamia klabu cha soka cha Morocco kiitwacho Wydad AC.
Safari yake ya Kazi Baada ya Kuondoka Yanga
Baada ya kuondoka Yanga, alikwenda Wydad Casablanca, Morocco.
Alisaini mkataba na vigogo hao wa ligi ya Botola Pro katika msimu wa 2024/25, ambapo alicheza mechi chache, zikiwemo za Kombe la Dunia la Vilabu la FIFA 2025.
Mnamo Januari 2026, Wydad ilimhamisha Aziz Ki hadi klabu ya Al-Ittihad SC Tripoli inayoshiriki Ligi Kuu ya Libya.
Baada ya muda mfupi nchini Libya, Aziz Ki alikamilisha rasmi urejeo wake Yanga kwa kishindo, akisaini mkataba wa miaka miwili wa kujiunga tena na klabu hicho cha Tanzania.
Februari 2025, miezi mitatu kabla ya kuondoka Yanga SC, Aziz alifunga ndoa na mwanadada maarufu nchini Tanzania Hamisa Mobetto, huku wengi wakidhania kwamba sababu kuu ya kurejea Tanzania ni kuwa na mke wake.