Watu 111 wafariki kwenye tetemeko la ardhi Colombia

Kulingana na Huduma ya Jiolojia ya Colombia, tetemeko hilo la kipimo cha 7.4, ndilo lenye nguvu zaidi kutokea nchini humo karne hii.

Tom Mathinji
1 Min Read
Watu 111 wafariki kwenye tetemeko la ardhi Colombia.

Takriban watu 111 wamefariki na wengine zaidi ya 100 hawajulikani waliko, baada ya tetemeko la ardhi kukumba Colombia.

Kulingana na Huduma ya Jiolojia ya Colombia, tetemeko hilo la kipimo cha 7.4, ndilo lenye nguvu zaidi kutokea nchini humo karne hii.

Tetemeko hilo la siku ya Jumatatu, liliathiri miji ya Magharibi ya nchi hiyo, ikiwa ni pamoja na Cali, Pereira, Quibdo na Manizales, huku likisikika katika nchi jirani za Ecuador Panama.

Tetemeko hilo ambalo limejiri chini ya miezi miwili baada ya mitetemeko mingine miwili kukumba maeneo ya Venezuela, na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 6,100, Kitovu chake kimetajwa kuwa San José del Palmar, katika eneo la Chocó, takribni kilomita 400 magharibi mwa mji mkuu Bogota.

Mkasa huo umejiri siku chache baada ya Abelardo de La Espriella kuapishwa kuwa rais, na kuweka utawala wake kwenye mtihani wa kwanza kuushughulikia.

Share This Article