Kenya ilimaliza ya pili katika mashindano ya Riadha Duniani kwa chipukizi chini ya umri wa miaka 20, yaliyokamilika jana uwanjani Hayward jimbo la Oregon nchini Marekani kwa medali 11,dhahabu 4 fedha 4 na shaba 4.
Washindi wa dhahabu za Kenya walikuwa Wilson Chepkwech, Josephine Mancha (1500m), Frankline Kibet (3000m), na Emmanuel Kiprono (5000m).
David Kapaiko alishinda fedha ya mita 1500 pamoja na Emmanuel Lemiso na nahodha Captain Nehemiah Kipngeno katika mita 3000 kuruka viunzi na maji na mita 5000 mtawalia.
Caren Chepchirchir alishinda nishani ya shaba ya mita 1500,huku Nicholas Losiwareng na nahodha mwenza Joyline Chepkemoi wakitwaa shaba za mita 3000 kuruka viunzi na maji na 5000 mtawalia.
Matokeo ya mwaka huu yalikuwa bora kuliko ya mwaka 2024 mjini Lima, Peru, ilikomaliza ya tano kwa dhahabu 3 fedha 3 na shaba 1.