Bodi ya Sukari yaagizwa kusitisha uagizaji sukari kutoka nje

Waziri Kagwe amesema kwa sasa Kenya ina hifadhi ya kutosha ya sukari, ambayo haitayumbisha soko la nyumbani.

Tom Mathinji
1 Min Read
Mutahi Kagwe - Waziri wa Kilimo na Ustawi wa Mifugo

Waziri wa Kilimo na Ustawi wa Mifugo Mutahi Kagwe, ameagiza Bodi ya Sukari ya Kenya kusitisha utoaji leseni za uagizaji sukari kutoka nje ya nchi, kwa misingi kwamba kuna sukari ya kutosha hapa nchini.

Kulingana Kagwe, kwa sasa Kenya ina hifadhi ya kutosha ya sukari, ambayo haitayumbisha soko la nyumbani.

“Nimeagiza Bodi ya Sukari ya Kenya kusitisha utoaji leseni za uagizaji sukari. Kuanzia sasa sitaki leseni zozote zitolewe za uagizaji sukari. Kiwango ambacho tumezalisha kinatosha. Hatutaagiza sukari na kuhatarisha viwanda vya hapa nchini,” alisema Kagwe.

Takwimu kutoka Wizara ya kilimo inaonyesha kuwa uagizaji sukari kutoka nje umepungua kutoka metrik tani 210,000 mwaka 2025, hadi metrik tano 60,000 mwaka 2026.

Kagwe alisema inalinda uzalishaji hapa nchini, huku Kenya inapojiandaa kutoka kwa taifa linaloagiza sukari hadi kwa taifa linalouza nje sukari.

Wakati huo huo Kagwe alisema serikali inajizatiti kukamilisha madeni ya kihistoria yanayodaiwa na wakulima wa miwa, akisema kati ya deni la shilingi bilioni mbili linalodaiwa na wakulima hao, ni shilingi milioni 265 pekee ambazo hazijalipwa.

“Furaha yangu itakuwa siku ambayo serikali haitakuwa na madeni ya wakulima,” alidokeza Waziri Kagwe.

Share This Article