Mamia ya wafanyabiashara wakadiria hasara Mlolongo

radiotaifa
1 Min Read

Mamia ya vijana wa eneo la Car Wash, Mlolongo wanakadiria hasara baada ya vibanda vyao vya biashara kubomolewa usiku na maafisa wanaodaiwa kuwa wa Mamlaka ya Kitaifa ya Barabara ( KeNHA ) bila notisi ya ubomozi.

Wafanyabiashara hao wamedai maafisa wa KeNHA walivamia vibanda vyao usiku wakitumia vijana na maafisa wa polisi katika kile wanasema ni njama ya mamlaka hiyo kuwaondoa eneo hilo na kuletaa wateja wapya.

Wakishangaa ni kwa nini eneo hilo libomolewe na ilhali maeneo mengine ya barabara ya Nairobi na Mombasa yangali yanamilikiwa na wafanyabiashara wa kando ya barabara.

Aidha, katika ubomozi huo wa pili sasa, kibanda kimoja kilisalia bila kubomolewa kikidaiwa kumilikiwa na bwanyenye mmoja ambaye amekuwa akishirikiana maafisa wa ngazi za juu wa mamlaka hiyo eneo hilo.

Juhudi za kupata taarifa kuhusu ubomozi huo ziliambulia patupu baada ya maafisa wa KeNHA Athiriver kukwepa kutoa majibu au kupokea simu.

Taarifa ya Jonathan Musau 

Share This Article