Trump kwa Iran: Hii ndio fursa ya mwisho kusaini ‘waraka mzuri’

Martin Mwanje
1 Min Read
Rais wa Marekani, Donald Trump / Picha kwa hisani ya BBC

Rais wa Marekani Donald Trump ameikosoa Iran kwa kukataa kufanya mazungumzo ya moja kwa moja. 

Amesema mazungumzo yanayolenga kusitisha mapigano kati ya nchi hizo mbili yanaendelea.

Akiwahutubia wanahabari jana Jumatatu, Trump alitaja hii kuwa “fursa ya mwisho” kwa nchi hiyo ya Mashariki ya Kati kusaini kile anachokiita “waraka mzuri.”

“Nafikiri labda tutapata kitu, ila nataka kuwapatia kila fursa ya mwisho kabla ya kuiharibu kabisa,” alisema Trump ambaye alionekana kuitishia Iran.

Rais huyo wa Marekani ameashiria kwamba mazungumzo yanayoendelea yanafanyika kwa ombi la Iran, chini ya upatanishi wa Qatar, Saudia, na nchi zingine.

Alisema Marekani na Iran wanajadili kuhusu kufunguliwa kwa Mlango Bahari wa Hormuz kufikia Agosti 4.

Awali, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Esmaeil Baghaei alikanusha kufanyika kwa mazungumzo yoyote na Marekani akiashiria kuwa nchi yake imekuwa ikifanya mazungumzo na Oman.

Share This Article