Mudavadi: Serikali kuunga mkono ushirikiano unaolinda mazingira

Mkuu huyo wa Mawaziri anasema juhudi za kusafisha Mto Nairobi zinahitaji ushirikiano wa pamoja katika taasisi zote za serikali.

Tom Mathinji
1 Min Read
Mkuu wa Mawaziri Musalia Mudavadi akutana na mwenyekiti wa tume ya kuboresha Mto Nairobi Kasisi Margaret Wanjiru.

Mkuu wa Mawaziri Musalia Mudavadi amesema serikali itaendelea kuunga mkono ushirikiano unaolinda mazingira na kusafisha Mto Nairobi.

Amesema juhudi za kusafisha Mto Nairobi zinahitaji ushirikiano wa pamoja katika taasisi zote za serikali hususan wakati huu ambapo kuna uwezekano wa mvua za El Nino.

“Mkutano wetu uliangazia kuboresha Mto Nairobi, kuimarisha afya ya umma, kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi pamoja na kuhakikisha mazingira safi,” aliongeza Mudavadi.

Aliyasema hayo aliposhiriki mazungumzo na mwenyekiti wa tume ya kuboresha Mto Nairobi, Kasisi Margaret Wanjiru pamoja na wanachama wa kamati yake.

Alidokeza kuwa serikali itapiga jeki juhudi za kuhakikisha Mto Nairobi inakuwa rasilimali muhimu sasa na pia katika vizazi vijavyo.

Share This Article