Chad yatangaza kujiondoa kutoka mahakama ya ICC

Uamuzi wa Chad unafuatia ule wa nchi jirani za Burkina Faso, Mali na Niger, ambazo pia ni serikali za kijeshi. 

Tom Mathinji
1 Min Read
Chad yatangaza kujiondoa kutoka mahakama ya ICC.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Chad imetangaza kuwa imemwandikia Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, ikimfahamisha nia ya kujiondoa kutoka kwa Mahakama ya Kimataifa kuhusu Uhalifu (ICC), 

Tangazo hilo la siku ya Jumatatu, limeifanya Chad ambayo ni serikali ya kijeshi, kuwa nchi ya hivi punde zaidi kutanagaza kujiondoa kwenye mahakama hiyo yenye Makao Makuu Jijini The Hague, lililobuniwa kushughulikia makosa ya kivita, uhalifu dhidi ya binadamu na mauaji ya halaiki.

“Hatua hii inajiri baada ya uchunguzi wa kina kuhusu majukumu ya mahakama ya ICC tangu ilipobuniwa mwaka 2002,” ilisema serikali ya kijeshi ya Chad.

Huku ikielezea kutoridhishwa na utendakazi wa ICC, Serikali ya Chad ilisema mahakama hiyo haifanyi kazi jinsi inavyotarajiwa na imekuwa ikishughulikia baadhi ya mataifa kwa namna isiyo sawa na kudai kwamba inalenga zaidi nchi za Afrika katika uchunguzi na kesi zake.

Uamuzi wa Chad unafuatia ule wa nchi jirani za Burkina Faso, Mali na Niger, ambazo pia ni serikali za kijeshi.

TAGGED:
Share This Article