Timu ya taifa ya soka ya wanawake ya Kenya-Harambee Starlets, iliwasili jijini Rabat, Morocco, Alhamisi jioni tayari kushiriki kipute cha Kombe la mataifa ya Afrika,WAFCON.
Starlets chini ya ukufunzi wa Beldine Odemba imekuwa katika kambi ya mazoezi nchini Ufaransa kwa takriban siku 10, zilizopita kujiandaa kabla ya kufunga safari kuelekea Morocco.
Kenya inayoshiriki dimba hilo kwa mara ya pili tangu mwaka 2016,itafungua kampeni yake dhidi ya wenyeji Morocco,Jumapili usiku kabla ya kukabiliana na Senegal Julai 30, na hatimaye kuivaa Algeria,Agosti 3.
Timu zitakazocheza hadi nusu fainali zitajikatia tiketi kwa Kombe la Dunia mwaka ujao nchini Brazil.
Aidha, timu nne zitakazoshindwa robo zitachuana kutafuta washindi wawili wa wakifuzu kwa mechi za mchujo baina ya mabara.