Mahakama ya kimataifa ya kutatua migogoro michezoni (CAS )imetenga Oktoba 8, kuwa siku ya kutoa uamuzi kuhusu kesi ya kubaini mabingwa wa Kombe la mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2025.
Kesi hiyo iliwasilishwa katika mahakama ya CAS na shirikisho la soka nchini Morocco.
Fainali hiyo ilisitishwa kwa zaidi ya dakika 10 kufuatia hatua ya wachezaji wa Senegal kuondoka uwanjani kupinga penati ya dakika za mwisho waliyopewa Morocco.
Kamatiya nidhamu ya shirikisho la soka Afrika CAF,ilidumisha ushindi wa Senegal wa bao moja kwa bila ,ila Morocco walitaka wachezaji wa Senegal wapokonywe ubingwa kwa kuondoka uwanjani kabla ya mechi kukamilika.