Idara ya Upelelezi wa Jinai, DCI imepiga hatua kubwa katika utoaji wa cheti cha maadili mema, yaani Certificate of Good Conduct, ambapo saa itachukua siku moja pekee kukipata cheti hicho.
Awali, utayarishaji wa cheti hicho uliichukua muda wa wiki nne au zaidi.
Hii ni kufuatia kuzinduliwa kwa mtambo mpya wa kielektroniki wa kutambua watu ujulikanao kama Multi Biometric Identification System (MBIS).
Wengi wa waliofika kutafuta cheti hicho baada ya kuzinduliwa kwa mtambo huo wa MBIS walisema iliwachukua takriban dakika tano pekee kukamilisha mchakato wote.
Itakuwa afueni kubwa wa wanaotuma maombi ya cheti hicho ambacho awali kilikuwa kero kwa wengi kutokana na mwendo wa kinyonga katika mchakato wa kukitafuta.