Serikali yazindua ujenzi wa makavazi ya Hayati Raila Odinga

Mradi huo unaotarajiwa kukamilika mwezi Oktoba mwaka huu utakuwa kivutio cha utalii na pia kufungua fursa za ajira pamoja na kuimarisha utamaduni.

Dismas Otuke
1 Min Read

Serikali imezindua ujenzi wa makavazi ya Hayati Raila Odinga nyumbani kwake Kang’o Ka Jaramogi katika eneo la Bondo, kaunti ya Siaya.

Hafla ya kuweka jiwe la msingi imeandaliwa Jumatatu ikiongozwa na Waziri wa Ulinzi Soipan Tuya na mwenzake wa Vyama vya Ushirika Wycliffe Oparanya.

Kiongozi wa chama cha ODM Oburu Oginga na  Raila Odinga Jr ni miongoni mwa jamaa waliohudhuria uzinduzi huo ambao ulifanyakika baada ya ibadi fupi ya maombi.

Makavazi hayo yatakayowekwa katika kaburi la marehemu, yanalenga kuhifadhi turathi yake kama njia ya kumbukumbuka na kutambua mchango wake katika ukuaji wa demokrasia nchini Kenya.

Mradi huo unaotarajiwa kukamilika mwezi Oktoba mwaka huu, utakuwa kivutio cha utalii na pia kufungua fursa za ajira pamoja na kuimarisha utamaduni.

Jengo hilo ambalo litakuwa na pembe tano litalandana na muungano wake wa kisiasa aliyoubuni wa Pentagon Alliance, uliowaleta pamoja viongozi kadhaa wa upinzani kwa lengo la kupigania uhuru wa kidemokrasia.

Share This Article