Uhispania watawazwa mabingwa wa Dunia baada ya miaka 16

Ni mara ya pili kwa Uhispania kunyakua Kombe la Dunia baada ya kutawazwa mwaka 2010.

Dismas Otuke
1 Min Read

Uhispania walinyakua Kombe la Dunia kwa mara ya pili baada ya kuwashinda Argentina bao moja kwa bila katika fainali ya makala ya 23 iliyoandaliwa Jumapili usiku uwanjani New York huko New Jersey, nchini Marekani.

Licha ya kumiliki mpira kwa takriban asilimia 70, Uhispania walishindwa kufunga bao ndani ya dakika 90, huku kipa wa Argentina Emiliano Martinez akikaa ange na kupangua zaidi ya mashambulizi tisa ya moja kwa moja.

Mabingwa wa mwaka 2022 waliokuwa wakiwinda kombe la nne walijipata taabani kufuatia kiungo Enzo Fernandez kupigwa kadi mbili za njano na kutimuliwa uwanjani mwishoni mwa dakika 90.

Uhispania waliendelea na bishabisha zao katika lango la Argentina na hatimaye kufumania nyavu dakika ya 107, Ferran Torres akiwajibika.

Ni mara ya pili kwa Uhispania kunyakua kombe hilo baada ya kutawazwa mabingwa wa mwaka 2010.

Share This Article