Ufaransa na Uingereza zitachuana Jumamosi usiku katika mechi ya kuwania nishani ya shaba katika makala ya mwaka huu ya Kombe la Dunia nchini Marekani.
Pambano hilo litasakatwa katika uwanja wa Miami kuanzia saa sita usiku ,timu zote zikitafuta medali baada ya kuambulia patupu katika harakati za kufuzu kwa fainali ya kesho.
Uingereza ilipoteza 2-1 dhidi ya Argentina wakati Ufaransa ikizimwa 2-0, na Uhispania katika hatua ya nusu fainali.

Itakuwa mechi ya nne kati ya timu hizo mbili ,Uingereza wakishinda mara mbili nao Ufaransa wakashinda mechi moja.
Kabla ya kushindwa katika nusu fainali,Ufaransa inayoongozwa na didier Deschamps ilikuwa na rekodi ya asilimia 100,wakati Uingereza yake Thomas Tuchel wakitoka sare kabla ya kushinda kupitia muda wa ziada dhidi ya Norway.